|
Written by Grace Mburu
|
|
Saturday, 14 August 2010 19:04 |
Siku mojaWakiongozwa na waziri wa elimu ya juu william ruto, wabunge hao wameelezea matumaini yao kuwa, serikali itatimiza ahadi yake ya kufanyia katiba mpya marekebisho. Aidha wanasema kuwa, kiu yao kuu ni kuwaona vinara wawili serikalini, waziri mkuu , Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki wakitimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni kuhusu katiba . Viongozi hao w a 'La' wlaikuwa wakizungumza walipoandaa karamu kwa wafuasi wao katika bustani ya arboretum humu jijini Nairobi. Ruto amesema kuwa, anaunga mkono kikamilifu utekelezaji wa katiba , Iwapo tu itafanyiwa marekebisho na kuwa, na manufaa zaidi kwa wananchi. Anasisistiza kuwa, ni sharti maslahi ya wakenya milioni 2.7 waliopinga katiba yashughulikiwa haraka iwezekanavyo. Ruto pia amepuuzilia mbali vitisho vinavyotolewa na wabunge kutoka chama cha ODM vya kumsimamisha kazi kama waziri, sawia na wenzake serikalini waliokuwa wakipinga katiba mpya. Ruto amesema kuwa, uugwana ni kujadili maswala wala siyo kujadili watu binafsi . mnamo siku ya alhamisi, katibu mkuu w a ODM, Nyang' Nyong'o alisema kuwa, hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wafuasi wa ODM waliopinga katiba mpya. Duru zinaarifu kuwa,rais Mwai Kibaki na Waziri mkuu Raila Odinga ameitisha kikao na wabunge , kitakacho =fanyika mnamo siku ya jumatatu kuzima uwezekano wa tofauti kali ambazo huenda zikaibuka pindi bunge litakapo buni kaamati maalum itakayoongoza utekelezaji wa katiba. |